BAADA ya hivi karibuni msanii wa muziki Bongo, Hamis Baba ‘H-Baba’ kuonyesha kuwa kammiss sana aliyewahi kuwa mpenzi wake, Irene Uwoya, mzazi mwenzake na msanii huyo, Flora Mvungi amevunja ukimya juu ya hilo. H-Baba juzikati kwenye ukurasa wake wa Instagram aliweka picha ya Irene kisha kuandika kuwa amemmisi, jambo lililowashangaza wengi kwani siku za nyuma kidogo aliwahi kumponda na kusema haoni ndani kwa Flora.
Kufuatia posti hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Flora na kumuuliza amejisikiaje baada ya baba wa watoto wake kuonesha hisia kwa zilipendwa wake, ambapo alisema:“Watu wanakuza mambo sana, mbona ni hali ya kawaida sana, ni kumbukumbu tu ambazo mtu zinamrudia, anafanya anachojisikia, ameona ni vyema kushea kumbukumbu zake na watu kwenye mitandao, sijaona shida yoyote na wala sijahisi wivu,” alisema Flora.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments