Meneja wa klabu ya Manchester City Mhispania Pep Guardiola amefunguka mengi baada ya kocha aliyekuwa jirani yake Jose Mourinho kuamua kuikacha Manchester United kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo katika msimu huu. Mhispania huyo amefunguka katika press aliyofanya katika mtanange wa Manchester city dhidi ya Leicester ambayo Man City walifanikiwa kuvuka hatua inayofuata baada ya mikwaju ya penati kumalizika kwa kujipatia penati 3-1, baada ya muda wa kawaida mcheezo huo kumalizika kwa vilabu hivyo kufungana goli 1-1. Guardiola amefunguka hayo na kumtetea kocha mwenzake baada ya kuulizwa anajisikiaje kumuona jiarani yake Mourinho kuondoka United,Guardiola alisema:- ” Niko upande wake, kama mameneja tuko wapweke sana,wenye timu wanatupa kazi sisi ili timu ziweze kupata ushindi na unaposhindwa kushinda najua kinachoenda kutokea, kila mara narudia kusema mimi nakuwaga upande wa mameneja siku zote, na kiukweli najua wanavyojisikia na najua niko hapa kwa sababu ya hali tuliyonayo, lawama zote ziko mikononi mwetu, lakini yeye ana uzoefu mkubwa , ni kati ya makocha wakubwa sana na nina uhakika atarudi kazini siku sio nyingi na nina uhakika tutapambana tena uwanjani, anafundisha vizuri sana, pia ni aibu sana lakini pia ni wakati mzuri kwa sasa, kikubwa tuseme tu asante sana kwa mashabiki wetu kwa kuja uwanjani ”
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments