Kaka wa msanii Irene Uwoya Atoboa Siri Nzito Kuhusu Ndoa ya Dogo Janja na Dada Yake

Kaka wa msanii Irene Uwoya Atoboa Siri Nzito Kuhusu Ndoa ya Dogo Janja na Dada Yake
Kaka wa msanii Irene Uwoya anayejulikana kwa jina la Babuu Uwoya, ametoa siri ya ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya ambayo ilikuwa ikifichwa kwa muda mrefu pasipo watu kuweza kufahamu


Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Babuu amesema kwamba familia nzima ya Uwoya hakuna ambaye alimkubali Dogo Janja kuwa mume wa mtoto wao, na ndio maana hawakuweza kuhudhuria siku ya harusi.

Babuu aliendelea kuelezea kuwa kitu ambacho anatambua ni kwamba Dogo Janja alikuwa rafiki yake mkubwa, na pia alisoma na wadogo zake, lakini hajawahi kumkubali kama shemeji yake, na kwamba familia ilikuwa inamtambua Ndikumana peke yake.

“Hakuna hata mmoja aliyependezewa na hilo suala, na hakuna hata mmoja aliyekuwepo kwenye harusi, sidhani kama ni ndoa, Dogo Janja alikuwa rafiki yangu, kasoma na wadogo zangu, hajawahi kuwa shemeji, mimi shemeji yangu namjua mmoja tu kashatangulia mbele za haki, anaitwa Ndikumana”, amesema Babuu.

Hata hivyo Babuu amesema suala la dada yake kuolewa na Dogo Janja haliwezi kuwaingia akilini, kwani dada yake alishafunga ndoa Kanisani na Ndikumana, ambayo huwa haivunjiki.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini