Muda mchache baada ya kocha Jose Mourinho kutimulia ndani ya Manchester United, mchezaji ghali zaidi ndani ya timu hiyo Paul Pogba ameonesha kufurahishwa na uamzi huo.
Kupitia mtandao wa Twitter Pogba ameweka picha iliyoambtana na ujumbe unaotaka wafuasi wake kuweka maoni yao juu ya picha hiyo. Hata hivyo Pogba aliifuta picha hiyo baada ya muda mfupi.
Naye mkongwe wa klabu hiyo ambaye pia ni kocha, Gary Neville ameunga mkono ujumbe wa Pogba kwa kuuandika na kuweka kwenye ukurasa wake.
Vyanzo mbalimbali pia vinataja makocha kadhaa ambao wanaweza kuchukua nafasi ya Mourinho mwisho wa msimu huu baada ya klabu kuweka wazi kuwa kocha wa muda atakayetangazwa ndani ya saa 48 atadumu hadi mwisho wa msimu.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments