Uongozi wa Simba umesema kuwa utabadilisha kikosi kitakachovaana na wapinzani wao KMC kesho katika uwanja wa Taifa ili kuwapa nafasi wachezaji wengine kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Nkana FC ya Zambia.
Simba kesho wanakibarua cha kucheza na KMC katika mchezo wa ligi kuu ikiwa ni kiporo chao kutokana na kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema wanatambua wana kazi nzito ya kutetea ubingwa na kuweza kusonga mbele kwenye hatua ya makundi hivyo wamejipanga kuweza kupata matokeo.
"Tuna kazi ya kucheza na KMC kesho, tunawaheshimu wapinzani wetu na tunatambua ushindani uliopo ila tumejipanga kupata matokeo katika mchezo huo na tutabadili kikosi chetu.
"Tutawapa nafasi wachezaji wetu kwenye kikosi ili wengine waendelee na maandalizi dhidi ya Nkana FC ya Zambia, sapoti ya mashabiki ni muhimu katika hili," alisema.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments