Sina Mpango na Mambo ya Ndoa na Wala Sifikilii- Linah

Sina Mpango na Mambo ya Ndoa na Wala Sifikilii- Linah
Mwanamuziki wa Bongo fleva mrembo Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hana mpango wa kuolewa na wala hawazi kuhusu mambo ya ndoa.

Linah amefunguka kuwa maisha ya ndoa kwa sasa hayafikirii na badala yake anatamani kuona muziki wake unampa heshima kwanza.




Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA, Linah alisema, licha ya wanawake wengi kutamani ndoa lakini kwake inekuwa tofauti na badala yake ameelekeza nguvu zaidi kwenye kazi zake.

Mimi ukiniuliza mambo ya ndoa kwa sasa ni ngumu kueleza.. niulize muziki wangu unakwendaje au kuhusu mwanangu”.

Linah amezaa Mtoto mmoja na mwanaume ambaye alikuwa kwenye mahusiano naye ya muda mrefu aitwaye Shaban Mchomvu ambaye amezaa naye Mtoto mmoja wa kike anayeitwa Tracey Paris.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini