Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hawatavumilia uvunjani wa haki za watu bali inapaswa kupingwa kwa njia za Kisiasa ikiwezekana kwenda Mahakama za Kimaitafa.
Akizungumza na waandishi wa habari Maalim Seif kuhusu imani yake kwa Mahakama ya Tanzania endapo haitotenda haki, zipo mahakama nyingine za Kimataifa ikiwemo ya Afrika Mashariki, Mahakama ya Afrika na ICC ambapo wanaweza kuchukua hatua ya kwenda.
“Uvunjani wowote wa haki za watu tusivumilie hivi hivi tupinge kwa njia nyingine za Kisiasa, twende mahakama za nje ya nchi za Kimataifa,”amesema Maalim Seif kwenye mkutano uliohusisha vyama sita vya upinzani nchini.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments