Wajumbe wa CAF Wawasili Tanzania kwaajili ya Ratiba Ya Michuano Ya Afcon U17 Mwaka 2019 Itakayofanyika Tanzania

Wajumbe wa CAF Wawasili Tanzania kwaajili ya Ratiba Ya Michuano Ya Afcon U17 Mwaka 2019 Itakayofanyika Tanzania
Shirikisho la soka Afrika CAF Leo Alhamisi ya Disemba  20 2018 katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam watapanga Makundi ya michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2019 kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambapo michuano hiyo inachezwa Tanzania wakiwa wenyeji.

Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo amesema kwamba maandalizi yote yamekamilika kuelekea zoezi hilo.

Ndimbo amesema kwamba Rais wa TFF, Wallace Karia tayari amepokea ugeni kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambao upo nchini kwa upangaji wa ratiba.

Amesema ujumbe huo wa CAF ukiwa hapa nchini umetembelea kukagua uboreshaji wa miundo mbinu ya viwanja unaoendelea na Karia amesema baada ya kutazama maendeleo ya Viwanja watashauri zaidi kulingana na walivyoona maendeleo hayo.

Ndimbo amesema mbali na Viwanja ujumbe huo wa CAF umetembelea Hoteli na Hospitali na leo utahudhuria upangaji wa ratiba ya fainali hizo utakaofanyika kuanzia saa 12:00 jioni na Dunia itapata kushuhudia upangaji huo moja kwa moja kwenye Televisheni.

Wajumbe wa CAF waliopo nchini ni Samson Adamu,Yasmin Hossam Eldin El Ehwany,Amri Ali Sadek,Mohamed Bakeer,Fayrouz Mahml,Mohamed Alaa El Shizy,Dina Medat,Moses Magogo anayewakilisha Kamati y Utendaji ya CAF wakati Leodger Tenga Mjumbe wa Kamati ya Utendaji CAF atakua mwenyeji wao.

Timu zilizofuzu kushiriki AFCON U17 Mei mwakani pamoja na wenyeji, Tanzania nyingine ni Morocco, Senegal, Guinea, Nigeria, Cameroon, Uganda na Angola.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini