Krissmas Kitaifa Kuadhimishwa Jijini Mwanza

Krissmas Kitaifa Kuadhimishwa Jijini Mwanza
Wakati zikiwa zimesalia siku sita tu kuelekea Sikukuu ya Krismasi, maadhimisho ya Sikukuu hiyo Kitaifa yatafanyika katika Jimbo Kuu Katoliki Mwanza.

Taarifa ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) iliyotolewa na Mratibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano, Pascal Mwanache imesema maadhimisho hayo yatatanguliwa na mkesha wa Krismasi utakaofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania Bugando.

Misa ya mkesha itaongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda ambaye pia ni msimamizi wa Kitume wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande.

“Aidha misa takatifu ya Krismasi Desemba 25, 2018 itakayoanza saa nne kamili asubuhi itafanyika katika kanisa la Epifania Bugando na pia itaongozwa na Askofu Renatus Nkwande,” imesema taarifa hiyo.

Baraza hilo limewaalika waumini wa dini hiyo kuungana katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambaye ni mkombozi wa ulimwengu.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini