Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Dudu Baya amemjibu Waziri Mwakyembe aliyetaka Jeshi la Polisi limkamate kwa kosa la kumdhihaki marehemu Ruge Mutahaba.
Dudu Baya kupitia video aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, amemtaka Waziri Mwakyembe kutosumbua Askari, bali wamwambie ni kituo gani anatakiwa akaripoti na yeye yupo tayari.
Mapema asubuhi ya leo Februari 26, 2019. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameliomba BASATA kumchukulia hatua Dudu Baya na Jeshi la Polisi limkamate.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA




0 Comments