Kaburi la Ruge Mutahaba Laanza Kuandaliwa | ZamotoHabari.


Maandalizi ya kumzika marehemu Ruge Mutahaba katika kijiji cha Kiziru Wilaya ya Bukoba yamepamba moto na ujenzi wa kaburi umeanza leo.
 
Siperatus Mbeikya ambaye ni mmoja wa wanafamilia amesema taratibu zinaendelea ikiwa ni pamoja na kupokea wageni kutokana maeneo mbalimbali.

Pia, amesema maandalizi hayo yamekwenda sambamba na kukubaliana na kikosi cha usalama barabarani sehemu utakapopita msafara wenye mwili wa marehemu Ruge.

Pilikapilika zimeongezeka katika eneo la msiba ikiwa ni pamoja na kumwaga vifusi kwenye maeneo korofi.

Marehemu Ruge anatarajiwa kuzikwa Jumatatu, wakati  mwili wake utawasili Dar es Salaam kesho Ijumaa na kuagwa Jumamosi.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini