Lowassa Afika Nyumbani kwa Ruge Mutahaba Kutoa Pole na kuwafariji wafiwa | ZamotoHabari.

Lowassa Afika Nyumbani kwa Ruge Mutahaba Kutoa Pole na kuwafariji wafiwa
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa leo asubuhi wamefika nyumbani kwa Prof. Mutahaba ambaye ni baba mzazi wa Ruge Mutahaba aliyekuwa mkurugenzi wa uzalishaji vipindi wa Clouds Media Group kutoa pole na kuwafariji wafiwa.

Ruge Mutahaba Alifariki dunia Juzi nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu ya figo zilizoanza kumsumbua mwaka jana.

Mwili  unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam kutokea Afrika Kusini siku ya kesho Ijumaa, Machi 1, 2019.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini