WAKATI sakata la nguli wa Muziki wa R&B, R Kelly la kutoka kimapenzi na mabinti wadogo bado likiwa la moto, baba wa staa wa Hip Hip, Drake, Dennis Graham ameibuka na kumtetea.
Dennis ambaye naye ni msanii wa muziki alimtetea nguli huyo alipokuwa akifanyiwa mahojiano ya wimbo wake mpya wa That On That; “Ni rafiki yangu mkubwa. Namtakia mema huko alipo.
Nachukia sana kinachoendelea kumtokea. Lazima kutakuwa na sababu ya mabinti hao kujitokeza. Lakini namsapoti kwa asilimia 100,” alisema Dennis.
R. Kelly anadaiwa kutoka kimapenzi na mabinti watatu wenye umri kati ya miaka 13 na 17. Hivi karibuni alikamatwa na Polisi wa Kituo cha Chicago nchini Marekani baada mkanda wa video kuonesha tukio zima lililotokea mwaka 1998.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments