“Zamaradi Moyo Wangu Unaumia Kwa Ajili Yako”- Zari | ZamotoHabari.

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ameibuka na kumtumia salamu za rambi rambi Zamaradi Mketema Baada ya Ruge Kufariki.

Marehemu Ruge Mutahaba alikuwa kwenye mahusiano na Zamaradi Mketema kwa miaka mingi na  kufanikiwa kuzaa naye Watoto wawili wadogo.


Tangu Ruge amefariki Zamaradi amekuwa akionekana mwenye majonzi na hasa kwa sababu baba wa Watoto Wake amefariki.

Zari amemtumia salamu za kumfariji Zamaradi kwa sababu na yeye mwaka jana alifiwa na baba wa Watoto Wake watatu Ivan Semwanga.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari ameweka picha ya Zamaradi na Watoto Wake wakiwa kwenye msiba na kuandika maneno machache “My heart bleeds for you Zama”.





Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini