CHECHE KURUDISHA SOKA LA PASI NA KASI KWENYE KIKOSI CHA AZAM | ZamotoHabari

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BENCHI la ufundi la muda la Azam FC kwa sasa linafanya kazi kubwa ya kurudisha aina ya mpira uliozoeleka kwenye timu hiyo wa kucheza soka la pasi na kasi uwanjani.

Kwa muda wa wiki moja sasa, kikosi cha timu hiyo kipo chini ya makocha wa muda Meja Mstaafu, Abdul Mingange na Idd Nassor Cheche, wakishika nafasi hizo baada ya kustitishiwa mikataba kwa makocha Hans Van Der Pluijm na Msaidizi wake, Juma Mwambusi.

Wawili hao waneiongoza Azam katika michezo miwili na kuifanikisha timu hiyo kushinda na kuingia hatua ya nane bora Kombe la FA pamoja na ushindi wa goli kuu wa kwanza baada ya muda mrefu.

Katika mchezo wa pili dhidi ya African Lyon uliochezwa mwishoni mwa wiki hii Azam  walifanikiwa kupata ushindi wa goli 3-1 ukiwa ni muendelezo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), awali wakipata ushindi mwingine mnono walipoipiga Rhino Rangers 3-0 na kutinga robo fainali ya Kombe la FA.

Kocha wa muda wa timu hiyo Cheche amesema kwa sasa wanataka kurudisha aina ya soka la timu hiyo ili kuleta ushindani na usumbufu kwa timu pinzani kwenye mechi zinazokuja.

“Kwanza Azam ina aina yake ya mchezo ambayo ilikuwa inacheza tofauti, tunajaribu kurudisha mchezo wenye pasi nyingi na spidi ndio tunajaribu kupambana nao, kurudisha wachezaji warudi katika ile hali kuleta ushindani na usumbufu kwa timu pinzani, ndio kitu tunachokifanya sasa hivi, kunyanyua spidi ya wachezaji ambayo ilikuwa ipo chini,” alisema.

Akizungumzia kwa ufupi mchezo uliopita dhidi ya Lyon, Cheche alisema kiujumla ulikuwa ni mzuri huku akikiri kuwa kuna mambo madogo madogo wamekuwa wakizifanyia kazi ili kuondoa baadhi ya makossa yanayoonekana.

“Mchezo tulianza taratibu lakini kadiri tunavyokwenda tumeenda tikibadilika na kufuata yale maelekezo tuliyowapa na mabadiliko tuliyofanya katika kipindi cha pili yameweza kutusaidia kuleta mabadiliko ambayo yametupa ushindi,” alisema Cheche.

Baada ya kumaliza changamoto ya mchezo huo, Azam FC imerejea tena  t mazoezi leo Jumatatu tayari kuanza maandalizi ya mchezo ujao wa ligi, itakaocheza dhidi ya JKT Tanzania Machi 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini