RUVU SHOOTING YATOA ONYO KWA TIMU ZA LIGI KUU | ZamotoHabari


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BAADA ya ushindi wa goli  6-2 dhidi ya wachimba madini Mwadui FC, Ruvu Shooting wametoa onyo kwa timu za ligi  na kuahidi  kuzipapasa timu zote zinazokuja mbele yake

Ruvu shooting wamefanikiwa kuondoka na ushindi huo katika Uwanja wa Mlandizi Mkoani Pwani na uongozi wa timu hiyo ukijitapa na kusema mbinu za mwalimu zimeanza kujibu.

Mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) wa Ruvu Shooting utakuwa ni dhidi ya Singida United na utachezwa  Machi 17 katika dimba la Namfua mkoani Singida.

Akizungumzia mechi hiyo na zinazofuata, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kwa sasa hakuna atakayeweza kuwazuia kwani spidi yao ni kubwa mithili ya gari lililokata breki kwenye mteremko mkali.

"Ushindi huu kwetu ni ishara ya kuwa hakuna wa kutuzuia, Kama ni gari basi kwa sasa tunasema limewaka na linapita kwenye mteremko mkali na kuweza kuzuia spidi yetu sio kazi rahisi, mbinu za mwalimu kujibu ni matokeo ya kupata ushindi kwa wapinzani wetu,” amesema Bwire.

"Wachezaji wanatambua kazi yao na tayari akili zao zimejiweka sawa kwa ajili ya kuwapapasa Singida United na tutakuwa pale Namfua Singida Machi 7, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema Bwire.

Ruvu Shooting wanaweka rekodi mpya mzunguko wa pili baada ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye ligi msimu huu na pia mchezaji wao Fully Maganga aliondoka na Mpira baada ya kupiga hat trick ya kwanza kwa Ruvu.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini