DTB FC kucheza ligi ya mabingwa wa mikoa ya TFF | ZamotoHabari

Mchezaji wa timu ya DTB FC, Godfrey Wambura, akikabiliana na washambuliaji toka timu ya Buyuni FC katika mechi ya mwisho ya hatua ya Sita Bora ya ligi ya Kanda ya Dar es Salaam iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwananyamala B. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya benki ya (DTB FC) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanikiwa kufuzu katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayosimamiwa na Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF).



Timu ya mpira wa miguu ya benki ya (DTB FC) imefanikiwa kufuzu katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayosimamiwa na Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF).

DTB FC imepata nafasi hiyo baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Mbuyuni FC katika mchezo wa mwisho uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwananyamala B katika manispaa ya Kinondoni.

Timu hiyo imemaliza katika nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi tisa (9) baada ya kucheza mechi tano.Ubora wa Timu ya DTB umedhihirika baada ya kushinda michezo miwili (2), kutoka suluhu katika michezo mitatu (3) na kutokupoteza mchezo hata mmoja.

Timu nyingine zilizopata nafasi ya kuiwakilisha mkoa wa Dar es Salaam ni Pan African na Buyuni FC.Mbali ya timu hizo tatu, timu nyingine zilizoshiriki katika hatua ya Sita bora ni Kigamboni FC, Ungindoni FC na Panama.

Meneja wa timu ya DTB FC, Michael Lugalela amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya ligi ya mabingwa wa mikoa na kuwataka wasibweteke.

“Natoa shukrani kwa uongozi wa benki ya DTB kwa kuihudimia timu kuanzia kushiriki katika mashindano mbali mbali na mpaka kushiriki katika ligi ya mkoa na kufuzu kuwania nafasi ya kushiriki ligi daraja la pili ya TFF, tunajivunia na tumedhihirisha kuwa tunaweza,” alisema Michael.

Alisema kuwa bado wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanafanya vyema katika mashindano hayo ambayo ushirikisha timu bingwa kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini