Tamasha la Utamaduni Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyika Tanzania. | ZamotoHabari

Na Chalila Kibuda , Blog ya Jiamii


Watanzania wametakiwa kudumisha tamaduni zao ili zilete mvuto kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kukuza sekta ya utalii nchini kwa kuwa na tija ya maendeleo ya Taifa. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Maandalizi ya Tamasha la Nne la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Michezo, Utamaduni na Sanaa, Susan Mlawi amesemakuwa Tamasha limeandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (SADC) kwa lengo la kukuza sekta ya utalii nchini lakini pia kukuza lugha ya kiswahili katika nchi mbalimbali duniani.

Aidha Tamasha hilo litatoa fursa mbalimbali kwa wafanya biashara kuonyesha bidhaa zao ili kukuza uchumi wao.Tamasha litatoa hamasa kwa watanzania kuweka kipaombele katika utamaduni wao pasipo kuendeleza tamaduni za kigeni ambazo kwa sehemu zinaathiri tamaduni za kiafrika.

AmesemaTamasha litahusisha zaidi ya nchi sita(6) za Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda,Rwanda, Burundi na Sudani ya Kusini.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Taifa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Joyce Fisoo amesema kwenye Tamasha hilo kutakuwepo na maonyesho mbalimbali ikiwemo mafunzo kwa wadau mbalimbali, Ngoma za asili, Sanaa na michezo na filamu mbalimbali.Hivyo amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujionea fursa mbalimbali za kiuchumi na utajiri uliopo Afrika.

Fisoo amesema kuwa katika nchi wanaoshiriki wametakiwa kukata mshiki mmoja atakayepanda mlima Kilimanjaro.Kwa upande Kamishina Msaidizi wa Utamaduni wa Wizara ya Jinsia, Kazi na Maendeleo ya Jamii wa Uganda EuniceTumwebaze amesema kuwa amejifunza mengi katika tamasha lilifanyika nchini mwao lilipofungua fursa kwa vijana wa Uganda wasanii.

Amesema Tanzania nao waonyeshe umahiri katika tamaduni zao ikiwa ni pamoja na kutangaza utalii.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Tamasha la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fisoo akitoa maelezo kuhusiana walipofikia katika maandalizi ya tamasha la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Mchezo na Sanaa Susan Mlawi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na serikali ilivyojipanga katika kufanikisha Tamasha la Utamaduni litalonyika Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kamishina Msaidizi wa Wizara ya Jinsia, Kazi na Maendeleo ya Jamii nchini Uganda EuniceTumwebaze akizungumza kuhusiana na uzoefu wa tamasha lililopita nchini Uganda katika kuzunguka fursa kwa watu wa nchi hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Mchezo na Sanaa Susan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Tamasha la Nne la Utamaduni litalonyika nchini Septemba mwaka huu.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini