Freeman Mbowe na Esther Matiko Washinda rufaa ya dhamana yao dhidi DPP | ZamotoHabari.

Freeman Mbowe na Esther Matiko Washinda rufaa ya dhamana yao dhidi DPP
Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali pingamizi la Serikali kupinga Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko kusikilizwa shauri lao la kuomba kupewa dhamana katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam

Hivyo kesi ya Mh. Mbowe na  Matiko inarudi Mahakama kuu kwa ajili ya kusikilizwa kama ilikuwa halali kwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu kufuta dhamana zao au hapana.

Novemba 23, 2018 Jaji Wilbard Mashauri akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, alifuta dhamana ya Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Wawili hao walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa Kisutu kufuta dhamana yao ambapo rufani yao ilipangwa kwa Jaji Sam Rumanyika.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini