Malipo Yamkwamisha Pluijm Kuondoka Azam FC | ZamotoHabari.

Malipo Yamkwamisha Pluijm Kuondoka Azam FC

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Azam FC, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ameshindwa kuondoka nchini Tanzania kwa wakati mara baada ya kutimuliwa klabuni hapo kutokana na kusubiria malipo yake ambayo hajapatiwa.



Azam FC iliachana na Pluijm hivi karibuni kufuatia matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mechi zao tano ikiwemo kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba.



Akizungumza na Championi Ijumaa, Mratibu wa Azam FC, Philip Alando, alisema Pluijm ataondoka mara tu baada ya kupatiwa haki yake ambayo bado hajaipata.



“Kocha Hans bado yupo hapa nchini na hajaondoka ila anasubiri akishalipwa ndiyo aweze kuondoka, uongozi unafanyia kazi suala lake na wakati wowote kuanzia sasa mchakato utakamilika.



“Siwezi sema ni kiasi gani anatakiwa kulipwa lakini kila kocha atalipwa kulingana na mkataba wake kwa upande wake yeye Hans na msaidizi wake Juma Mwambusi,” alisema Alando.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini