Harmonize Atoa Siri Kuhusu EP Ya Afro Bongo | ZamotoHabari.

Harmonize Atoa Siri Kuhusu EP Ya Afro Bongo
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Harmonize amefunguka na kutoa siri kuhusu EP (Extended Playlist) yake ya Afro Bongo.

Wiki iliyopita Harmonize aliachia ngoma nne kwa Mpigo alizozipa jina la Afro Bongo Lakini jana  ametoa siri kuwa video za nyimbo zake nne zote zipo tayari.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameweka wazi kuwa tayari video za nyimbo zote nne akizoziachia ziko tayari.

MHH…!!! USICHOKIJUA NIKWAMBA
NGOMA ZOTE ULIZOZISIKIA KWENYE #AFROBONGO VIDEO ZAKE ZOTE ZIPO TAYALI BASI HAPA NILIVYOKAA NI KAMA MZEE YUSUFU YANI SINA PLESHAAA KWENYE TAALUMA YANGU …!! 🤣
OYAAA…!!! LINK PA BIO × @yemialade 🥁🎻🎶🎸 @krizbeatz_ LET’S GO …!!!”.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini