Moto Mt. Kenya: Wakulima wa bangi watuhumiwa kuwasha moto | ZamotoHabari.

Moto Mt. Kenya: Wakulima wa bangi watuhumiwa kuwasha moto
Moto unaodaiwa kuwashwa na wakulima wanaotaka kupanda bangi unatishia maelfu ya mahekari ya misitu ya mianzikatika Mlima Kenya au Mount Kenya.

Haki miliki ya pichaBOBBY NEPTUNE
Tayari moto huo umeharibu kilomita 80 mraba za ardhi yenye nyasi na sasa unatishia misitu ya jadi.

Misitu mikubwa ya mianzi inapatikana katika eneo la Afrika mashariki.

Kwa mujibu wa shirika la utafiti wa kimataifa wa ukulima CGIAR, ni sawa na takriban 3-4% ya misitu jumla ya mianzi au bamboo inayojulikana.

Haki miliki ya pichaBOBBY NEPTUNE
Moto huo, ulianza siku saba zilizopita, unateketea katika maeneo mawili na umekuwa ukisambaa kutokana na upepo na joto kali.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini