Mabango ya Wana BUKOBA kwa Diamond ni Kizungumkuti | ZamotoHabari.

Mabango ya Wana BUKOBA kwa Diamond ni Kizungumkuti
Mwili wa aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi vya Clouds radio na Clouds fm Bwana Ruge Mutahaba uliwasili siku ya jumapili katika kijiji chao huko Bukoba ambapo kabla ya kufika huko ulitembezwa katika baadhi ya mitaa ili kugawa na watu wa Bukoba.

watu wengi walijitokeza kwa ajili ya kuupokea mwili huo kutoa uwanja wa ndege mpaka kuusindikiza kufika nyumbani kwao Kisiru -Kabale ambapo ndipo atakapopumzishwa hapo.


Hata hivyo , mabango mengi yaliandikwa kuonyesha wasifu na mengi aliyokuwa akiyafanya Ruge lakini yapo pia yaliyokuwa yakitoa lawama kwa msanii Diamond .

Hali ya mtandaoni na akili mwa watu ni tete kwa sababu hakuna swala la wazi kwa nini watu wamekuwa wakimshambulia msanii Diamond  kuhusu kuudhuria katika msiba wa Ruge tangu siku ya kwanza.

Hakuna anaejua sababu iliyomfanya diamond kufanya hivyo , inawa hisia za watu wengi mitandaoni zinaonyesha kuwa Bifu lilokuwepo kati ya Ruge na Diamond ndilo lilimfanya Diamond kufanya hivi , lakini ni kitu mabacho hata yeye hajaonyesha kutaka kuzngumzia hilo.

Katika moja ya mabongo yaliyopigwa picha na kusambaa sana ni hili lilokuwa likisema “DIAMOND MUOGOPE MUNGU NA WEWE UTAKUFA TU, R.I.P RUGE”
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini