Mchungaji aliyetikisa dunia kwa habari za kufufua mtu Alph Lukau wa Afrika Kusini ameamua kuomba radhi kwa kufanya tukio hilo ambalo limekua likimuumiza.
Mchungaji Lukau amesema hayo wakati akizungumza na kituo cha redio cha Power FM cha Afrika Kusini, kwamba anaomba radhi kwa kuwa mtu ambaye alionekana akimfufua hakufa na alionekana kuwa hai kabla hajaletwa kanisani, na ndugu zake huenda walifanya hivyo wakiamini kuwa kuna kitu kinaweza kikatokea kwa ndugu yao ambaye alitangazwa kufariki.
“Kabla ya kuingia maeneo ya kanisa, sanduku lilianza kutikisika, ikimaanisha kuwa mtu alikuwa hai. Samahani sana kwa uwasilishaji mbaya wa ukweli, mtu alikuwa hajafa na hajawahi hata kuwa mochwari kama ilivyosemwa awali, tulikuwa kwenye nyumba ya Mungu na mimi ni mchungaji tu, lakini samahani hatukuwaambia watu ukweli tangu mwanzo. Nadhani ndugu zake walimleta kanisani wakiamini kuna kitu kinaweza kutokea kwa ndugu yao”, amesema Lukau.
Akiendelea na mahojiano katika kituo hicho cha redio, Mchungaji Lukau amesema kwamba ingawa hakumfufua mtu huyo, alikiri kuwa alishawahi kurudisha uhai wa mtoto ambaye alifariki tumboni mwa mama yake, baada ya mapigo yake ya moyo kutoonekana, na mara baada ya maombi yalirudi.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments