Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 26 nchini Ureno, amejifungua mtoto wa kiume siku ya Alhamisi licha ya kutangazwa kuwa ni mfu toka mwezi Disemba mwaka jana.
Mashine ya kumpa joto mtoto
Mwanamichezo wa kimataifa, Bi Catarina Sequeira alipatwa na shambulio kali la pumu akiwa nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Bi Sequeira mwenye umri wa miaka 26 amezikwa Ijumaa, siku moja baada ya mtoto kutolewa tumboni mwake.
Mtoto huyo aliyepewa jina la Salvador, amezaliwa baada ya kukua kwa wiki 32 tumboni mwa mama yake na sasa yupo chini ya uangalizi kwenye hospitali ya watoto.
upasuaji
Hii ni mara ya pili nchini Ureno kwa mtoto kuzaliwa kutoka kwa mama ambaye ni ‘mfu wa ubongo’.
Sequeira ambaye alikuwa mwanariadha wa mbio za mitumbwi amekuwa akisumbuliwa na pumu toka utoto wake.
Aliwahi kuiwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya kimataifa wakati wa uhai wake.
Shambulio lililochukua uhai wake lilimpata akiwa na mimba ya wiki 19, hali iliyomfanya kupoteza fahamu. Siku chache akiwa chumba cha wagonjwa mahututi hali ilizidi kuwa mbaya na akatangazwa kuwa ‘mfu wa ubongo’ Disemba 26. Madaktari wakamuwekea mashine ya kusaidia kupumua ili mtoto tumboni aweze kuishi. Mashine hiyo iliwekwa kwa siku 56.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments