Shirika la usafiri wa ndege nchini Rwanda limetoa agizo kwa marubani na kampuni za ndege kutoendesha ndege za Boeing 737 Max 8 na 9 katika anga ya Rwanda.
Rwanda sasa imejiunga na mataifa mengine duniani ambayo yamepiga marufuku usafiri wa ndege hizo za aina ya Boeing 787 Max 8 na Max 9.
Hii inafuata baada ya ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines ilioanguaka Jumapili muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu Addis Ababa na kusababisha vifo vya watu 157.
Taarifa zinaeleza kwamba Rwanda ilikuwa na mipango ya kukodisha ndege mbili za aina hiyo Boeing 737- 800.
Hatahivyo huenda mipango hiyo ikasitishwa kwa muda sasa wakati kukisubiriwa uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoanguka Jumapili nje kidogo ya mji mkuu Addis Ababa.
0 Comments