KATIKA kuelekea kwenye msimu wa siku kuu ya Pasaka Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wametangaza Promosheni na Ofa kubwa katika msimu huu wa sikukuu ya pasaka ambapo wateja wake wataweza kununua vingamuzi vya antenna kwa bei ya punguzo sambamba na kushuka bei ya baadhi ya vifurushi.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja masoko wa Startimes David Malisa amesema kuwa, "Tumejiwekea utaratibu wa kuwapatia wateja wetu na wale wanaotamani kuwa wateja sababu kufurahia zaidi kila sikukuu zinapofika, Msimu huu wa pasaka tunawaletea Promosheni ya Beba Beba na StarTimes na katika hili tumepunguza bei ya king'amuzi cha antenna kutoka shilingi 79,000 hadi kufikia awali shilingi 69,000 tu na mwezi mmoja bure kabisa kwa kifurushi cha UHURU" ameeleza Malisa.
Mbali na kupunguza bei ya kingamuzi cha Antenna StarTimes wamepunguza bei ya Kifurushi cha UHURU ambapo Malisa amesema kuwa,
"Pia tumepunguza bei ya kifurushi cha UHURU ambacho ni cha juu kabisa kwa watumiaji wa Antenna. Awali wateja walikuwa wakilipia shilingi 24,000 lakini kuanzia leo tarehe 15 Machi bei yake itakuwa Tsh 18,000 tu na Kifurushi hiki ndicho chenye chaneli zote za burudani, filamu, tamthiliya na michezo bila kupitwa hata na kimoja" amesema.
Aidha ameeleza kuwa
Katika kipindi chote cha Promosheni ya Beba Beba wateja wa StarTimes watafurahia maudhui ya kiwango cha juu ikiwemo ligi ya kandanda la Ulaya, Europa League ambayo bado inaendelea, tamthiliya za kuvutia kama Wildflower na Waaris.
Promosheni hiyo itaendelea hadi tarehe 31 ya mwezi Mei mwaka huu, huku wakiamini wateja wao watafurahia bei ya punguzo ya kifurushi cha UHURU, pia wamewataka wateja wanaotamani kujiunga na familia ya StarTimes inayokua kila siku kuwa huu ni wakati sahihi kabisa kwao kwani gharama zimekuwa nafuu kwa ajili yao.
Meneja masoko wa Startimes David Malisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Promosheni na ofa za msimu wa siku kuu ya Pasaka ambapo wateja wake wataweza kununua vingamuzi vya antenna kwa bei ya punguzo sambamba na kushuka bei ya baadhi ya vifurushi.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments