Real Madrid Yapokea Kichapo Kingine Kutoka Kwa Barcelona Ndani ya Siku 3 | ZamotoHabari.


Ushindi wa goli 1-0 wa Barcelona dhidi ya Real Madrid, unaifanya Barcelona kuwa timu ya kwanza katika Historia ya Ligi Kuu nchi Uhispania kushinda mechi nne mfululizo katika dimba la Santiago Bernabeu

Kutokana na goli pekee lililofunga na Kiungo Ivan Rakitic, Barcelona sasa inaendelea kuongoza ligi ikiwa na alama 60, alama 10 zaidi ya Atletico Madrid iliyo nafasi ya pili na alama 12 dhidi ya Real Madrid iliyo nafasi ya tatu

Ushindi huo unaifanya Barcelona kuongoza kuifunga Real Madrid kwa mara ya kwanza kwa miaka 88 katika michezo yote waliyocheza ambapo sasa imeshinda michezo 96 huku Madrid ikishinda michezo 95

Aidha, Kocha wa Madrid, Santiago Solari anakuwa Kocha wa kwanza kuinoa klabu hiyo na kushindwa kushinda katika michezo yake mitatu ya mwanzo dhidi ya Barcelona(L2 D1) tangu Leo Beenhakker aliposhindwa naye mwaka 1987(D2 L2)  -
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini