VIDEO: Rais Magufuli alivyookoa mamilioni yaliyokuwa yatumike kuweka nembo ndege ya Serikali

Rais John Magufuli ameelezea jinsi baadhi ya watumishi walivyotaka kutumia zaidi ya Sh200 milioni kuweka nembo kwenye ndege ya serikali iliyotolewa kwa ATCL ambapo nembo hiyo baadaye ilichorwa kwa shilingi milioni tano tu.

Rais amesimulia hayo leo Alhamisi March 27, 2019 Ikulu Dar Wakati akimuapisha balozi Mpya wa Cuba Valentino Mulowola.

"Nilipokuwa kwenye sherehe Uwanja wa ndege, nilitoa agizo ndege ya Rais itumike kubeba abiria, nikaambiwa kazi ya kuchora twiga na nembo ya Air Tanzania haiwezi kufanyika nchini, nikatajiwa nchi 3 ndio zinaweza kucjora, yaani hapa nchini haiwezekani.

"Gharama za kuchora twiga na nembo ya Air Tanzania nikaambiwa ni Mil. 200 za Tanzania na malipo ya awali kuhusu kazi hiyo yameshalipwa, nikasema ndege ikiondoka na nafasi zao wajue zimeondoka, ndege imebaki na kazi imefanyika nchini kwa Mil. 5"  Amesema Rais Magufuli

==>>Msikilize hapo chini



Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini