Waswahili husema ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni, Je unajua matumizi yote ya tumbaku ?
Mkoani Tabora nchini Tanzania wanawake wamekuwa wakitumia Tumbaku ili kupunguza hamu ya tendo la ndoa.
Huweka sehemu ya siri kisha kuitoa baada ya muda.
Tabia hiyo imezoeleka sana miongoni mwa wanawake wasio na wenza wao, ikiwemo wajane. Lakini kwa upande wa afya, wako salama?
Wanawake hususani wasio kuwa katika uhusiano na wanaume ama kuolewa hutumia njia kumaliza hamu zao.
''Mimi ni mjane, natumia tumbaku katika kumaliza hamu zangu kwa sababu sina mwanaume na wala sitaki mwanaume mwingine, kwa wiki naweka mara mbili''anasema Zaituni Shabani mmoja ya wanawake wanaotumia tumbaku sehemu za siri.
Wanawake wengine waliozungumza na mwandishi wa habari hizi kama Asha, si jina lake halisi anasema kuwa anatumia tumbaku kwa sababu alikimbiwa na mwanaume wakati ana ujauzito.
''Kwa kweli sitaki kusikia tena wanaume mi nitabaki na tumbaku, maana nikitumia hamu yote inaisha sina haja tena'' ,anasema Asha
Wanawake wanakiri kuwa matumizi ya tumbaku sehemu za siri huwasaidia kumaliza hamu ya tendo la ndoa.
TUMBAKU INATUMIWA VIPI SEHEMU ZA SIRI?
Kwa mujibu wa wanawake hawa huchukua majani makavu ya tumbaku kisha kutwanga na baada ya hapo huchanganya na mafuta kidogo pamoja na magadi, ama na mara nyingine hutumia ugoro kufanya mchangayiko huo. Baada ya hapo huweka sehemu za siri na kisha hupata muwasho ambao ndiyo humaliza haja ya tendo la ndoa.
''Mimi huwa napaka mara mbili kwa wiki na huwa naweka kwa muda kidogo kabla niondoe na kisha napata muwasho, na wala sipati maumivu yoyote nikimaliza matamanio yangu ya kufanya tendo la ndoa yanakuwa yameisha'',anasema zaituni.
Kwa kawaida wanawake hawa baada ya kupaka tumbaku ama ugoro sehemu za siri husikia kama wamekutana kimwili na wanaume.
WANAUME WANASEMA NINI?
Katika kijiji cha Ugala suala hili ni jambo la kawaida miongoni mwa wanawake lakini kwa upande wa wanaume si wengi wanajua , na wanaojua wanasema kuwa imekuwa siri baina ya wanawake.
"Mimi nimekuwa nikisia lakini mara nyingi ni kwa bahati mbaya wao wakiongea, na nikiwauliza , wanasema ni siri yao ni baina ya wanawake na si wanaume". Anasema mzee Usantu mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ugala.Image captionWataalamu wa magonjwa ya wanawake wanasema matumizi haya yana athari kiafya
KUNA ATHARI ZOZOTE KIAFYA?
Kwa mujibu wa baadhi ya wanawake wanaotumia tumbaku sehemu zao za siri, wanasema hawajawahi kupata tatizo lolote kiafya.
Lakini mtaalamu wa magonjwa ya akina mama anasema kuwa baadhi ya wanawake wanaokutwa na viashiria vya saratani hasa ya kizazi wamekuwa na historia ya kutumia tum
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments