MAMBO vipi mpenzi msomaji, kama kawaida nakuletea mastaa mbalimbali na maisha wanayoishi na watoto wao. Leo tunaye mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’ ambaye atafunguka kuhusiana na malezi ya wanaye wawili ambao ni Saida na Chonge.
Kumsikia Madee ungana nami kwenye mahojiano haya hapa chini…
Wikienda: Umekuwa ni baba wa tofauti kwa kulea watoto mwenyewe bila mama, ujasiri huu unaupata wapi?
Madee: Mwanaume yoyote yule akishapenda watoto lazima atapata ujasiri kama nilio nao mimi.
Wikienda: Kwa nini mpaka sasa hujaamua kuishi hata na mama wa mtoto mmoja?
Madee: Bado sijafikiria kwa sababu kuoa sio lelemama, nataka kuwa mfano, sitaki kuoa leo na kuacha kesho.
Wikienda: Mara nyingi nakuona na mtoto wako mdogo sehemu mbalimbali, vipi hakuzuii kufanya mambo yako?
Madee: Hapana tena ninapokuwa naye hata kwenye shoo zangu nafarijika sana kiuk-weli.
Wikienda: Nini unachokipenda kwa watoto wako?
Madee: Napenda kuwaona wakiwa pamoja kwa sababu nikiwaona wote wananiongezea siku za kuishi, nakuwa na furaha sana.
Wikienda: Wewe ni mwanaume na mara nyingi watoto wako wanaulamba nguo nzuri, nani anawachagulia?
Madee: Nawanunulia mwenyewe na kwa sababu mimi ni mtoto wa mjini, najua mambo mengi mno lazima niwachagulie vitu vikali.
Wikienda: Nini unachokitamani kwa watoto wako?
Madee: Napigana sana ili niwape elimu bora maana nataka wawe wasomi.
Wikienda: Unapoishi kuna dada wa kazi anakusaidia watoto?
Madee: Hapana, nafanya kazi zao na mimi najisikia fahari kufanya kila kitu kwa wanangu mwenyewe.
Wikienda: Watoto wako wote ni wa kike, hutamani upate wa kiume pia?
Madee: Mtoto ni mtoto hata kama ningekuwa na wa kike wote lakini ninaye wa kiume mmoja pia.
Wikienda: Asante sana kwa ushirikiano.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments