Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye amesema uamuzi uliochukuliwa na Edward Lowassa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) hauwezi kumshtua na kusisitiza kuwa yeye hawezi kufuatana naye katika safari hiyo.
Akizungumza na www.eatv.tv Sumaye ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu amesema kuwa uamuzi wa Lowassa haumpi shida acha aende na wao watabaki wakijenga chama.
“Mimi haunipi shida, mtu akiamua kuhama chama na kwenda kingine ni uamuzi wake na kama kaamua acha aende, sisi tutaendelea kujenga chama na unapozungumzia kuhama mimi kwangu ni ndoto ambayo haipo", amesema Sumaye.
Ikumbukwe Lowassa alitangaza kuondoka CCM, Juni 28 mwaka 2015 baada ya kueleza kutoridhika na mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya chama hicho kabla ya Machi Mosi 2019, kutangaza kurejea CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments