Hiki hapa Chanzo Cha Kifo cha Msanii Nipsey Hussle wa Marekani | ZamotoHabari.

Hiki hapa Chanzo Cha Kifo cha Msanii Nipsey Hussle wa Marekani
Kwa mujibu wa gazeti la 'New York Daily News' limesema kuwa chanzo kutoka Polisi kimewaambia Polisi wa Los Angeles(LAPD) wamepata mwongozo juu ya mtu anayeshukiwa kumpiga risasi Mwanamuziki Nipsey Hussle(33)

Chanzo kimeeleza mtu huyo alikuwa anafahamiana na Nipsey na anaaminika kuwa na uhusiano na makundi ya kihuni(gang) lakini hawakuwa maadui hivyo mauaji hayo yanachukuliwa kuwa ni njama zilizoenda vibaya

Hata hivyo, mauaji yanahusishwa na makundi hayo ya kihuni kwa sababu zamani Nipsey alikuwa na uhusiano na makundi hayo na kabla ya kifo chake siku ya Jumapili kupitia Twitter aliandika "Kuwa na maadui wakubwa ni baraka."

Nipsey aliuawa Jumapili majira ya saa 9:20 alasiri nje ya duka lake la nguo lililopo Slauson Ave, Los Angeles alikimbizwa hospitali ambapo mauti yalimkuta. Watu wengine wawili walijeruhiwa katika tukio hilo

Inaelezwa Mwanamuziki huyo alikuwa amepanga kukutana na LAPD siku ya Jumatatu kuzungumzia namna ya kuzuia vurugu zinazohusiana na makundi ya kihuni katika mitaa hiyo

Aidha, katika mitandao ya Kijamii kulienea taarifa kuwa huenda Nipsey ameuliwa na Mamlaka hususani CIA kutokana na kutaka kwake kutengeneza Makala kuhusu hukumu ya Dkt. Sebi ya mwaka 1985 aliyejinasibu kuwa alikuwa na uwezo wa kutibu UKIMWI na anayedaiwa kuuliwa na Mamlaka
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini