Wafanyakazi wa Kambi ya Wachina, wanaofanya kazi ya ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Rusumo wilayani Ngara wapata ajali | ZamotoHabari.

Kumetokea ajali ya basi dogo lililokuwa limebeba Wafanyakazi wa Kambi ya Wachina wanaofanya kazi ya ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera leo April 02/2019 majira ya asubuhi, taarifa zinaeleza watu wawili wamefariki na majeruhi wamekimbizwa Hospitali ya Murugwanza na Nyamiaga kwa matibabu zaidi.

Watu watatu wanasadikiwa kupoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa katika ajali ya gari la mafundi wanaotekeleza mradi wa kuzalisha umeme wa Megawati 80 kutoka kwenye maji ya Mto Kagera eneo la Rusumo Wilaya ya Ngara.

Majeruhi wamekimbizwa Hospitali ya Murgwanza na Nyamiaga kwa matibabu zaidi
Umeme huo unatarajiwa kutumika kwenye nchi tatu ambazo ni Tanzania, Rwanda na Burundi.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini