MABONDIA HUSSEIN PENDEZA NA JUMA RAMADHAN KUZICHAPA SIKU YA PASAKA | ZamotoHabari

 Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MABONDIA Hussein Pendeza na Juma Ramadhani 'Choki' wametamba kila mmoja kwa wakati wake kuibuka na ushindi katika mpambano kati yao ambao unatarajia kufanyika Aprili 21 mwaka huu ambayo itakuwa Sikukuu ya Pasaka.

Akizungumzia mpambano huo ambao utafanyika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam Juma Ramadhan 'Choki' amesema ana uhakika wa kushinda kwani hivi sasa yupo fiti mpaka mwenyewe anajiogopa kutokana na mazoezi ambayo ameyafanya kujiandaa na pambano hilo.

"Kwa namna ambavyo nimejiandaa , sio huyo tu Pendeza, yoyote ambaye atakuja mbele yangu atapokea kichapo tena cha mbwa mwizi.Hivyo wakae chonjo vingenevyo nitawararuaraua na sijaona katika uzito wangu wangu wa kilogramu wa kunisumbua kwani najiamini na ninajimini kwa mazoezi ambayo nimeyafanya,"amesema.

Hivyo Choki amewaomba mashabiki wake wa Manzese,Mabibo, Mbagala Kuu na Mtoni Kijichi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kumpa sapoti na anataka kuweka historia ya aina yake kwenye mpambano huo.

 Kwa upande wake bondia Pendeza amesema kuwa atahakikisha anampiga Choki kama begi kwani kwake ni mtoto mdogo sana katika ulimwengu wa masumbwi na kipigo ambacho atampatia atajuta kuzaliwa kwa kipigi ambacho atakipata.Pia ameongeza anawaomba mashabiki wake wote na wapenzi wa ngumi kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuangalia jinsi anavyo msambaratisha mpinzani wake.

Mpambano huo umeandaliwa na Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo amefafanua maandalizi yote muhimu yameshafanyika ."Pambano litafanyika Siku ya Sikukuu ya Pasaka,"amesema Super D.

Pia amesema bondia mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anayefanya shughuli zake nchini Australia  ndiyo aliyosababisha mabondia hao wazipige siku hiyo kwa kuwa vijana wanatakiwa kuendeleza rekodi zao za masumbwi kila wakati ndio maana akaongeza nguvu ili mpambano uho ufanyike

Super D ameongeza mbali na pambano hilo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayokuwa yanafanyika siku hiyo ambapo bondia  Idd Mkwera ataoneshana umwamba na Rojas Masamu wakati Shomari Milundi ataoneshana umwamba na Bakari Mbede.

Wakati Ibrahimu Makubi atavaana na Haruna Ndalo na Ramadhani Mbegu 'Migwede' atapambana na Rashidi Mnyagatwa na Salum Tandu zidi ya Gerald Mkude na Sunday Kiwale 'Moro Best' atalindima na Luckman Ramadhani Vicent Mbilinyi na Shabani Mbogo Hussein Shemdoe na Shehe Azizi na Ahmadi Kombo atakumbana na Sandali Nyambala

Mapambano yote hayo yanaletwa yanafanyika chini ya kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ambayo ipo nchini Tanzania kwa ajili ya kuinua vipaji ya vijana mbalimbali ili kuendeleza vipaji vyao pendwa na kupitia kampuni ya Super D Promotion imejizatiti kuweka angalau pambano moja kila baada ya miezi milili ili kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyao na kujiendeleza kupitia mchezo uho wa masumbwi nchini. 


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini