Polisi Kigoma Yaua Majambazi Watatu | ZamotoHabari.

Polisi Kigoma Yaua Majambazi Watatu
Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa huku askari polisi mmoja  akijeruhiwa baada ya kutokea kwa majibizano ya risasi katika tukio la ujambazi wilayani Kibondo mkoani Kigoma..

Inaelezwa majambazi hao  walikuwa wamejipanga kufanya uporaji katika baadhi ya nyumba za wananchi wilayani Kibondo.

Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Louis Bura, alisema juzi usiku   polisi walipokea taarifa kutoka kwa wananchi  kuwa kuna majambazi walikuwa wanataka kuvamia baadhi ya nyumba.

Alisema   walifika eneo la tukio na   kurushiana risasi ambako askari mmoja,     James Mwita (37) na mama mmoja, Sophia Dicksoni (60) walijeruhiwa na   wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Kibondo.

Alisema askari huyo alipatiwa matibabu ya awali na sasa   amepatiwa rufaa   kwenda  kwenye matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na majeraha ya mguuni.

DC aliwapongeza wananchi kwa kuendelea kuonyesha ushirikiano  kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa wanayo ifanya kwa kuwa ni kazi ngumu.

Amewataka wananchi kuacha kuwaingilia katika utendaji kazi wao kwa kuwa wapo baadhi wanawakamata wakiwatuhumu kwa ujambazi lakini ndugu zao wanawatetea na kudai siyo majambanzi.

Pia aliwataka wananchi kuacha kutoka nje   wanaposikia milio ya risasi kwa ajili ya usalama wao kwa kuwa ni hatari   kufuata milio hiyo inaweza sababisha madhara makubwa.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini