Marekani Yatoa Wito kwa Burundi Kuwafungulia BBC na VOA | ZamotoHabari.

Wizara ya Mambo ya nje nchini Marekani, imetoa wito kwa serikali ya Burundi, kubadilisha uamuzi wake wa kufungia matangazo ya Shirika la Habari la Sauti ya Amerika (VOA) na BBC.

Msemaji wa Wizara hiyo Robert Palladino ameitaka serikali nchini humo pia kuwaruhusu wanahabari wanaofanya kazi na mashirika hayo, kuwaacha kufanya kazi yao kwa uhuru kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Burundi imechukua hatua hiyo kwa madai kuwa mashirika hayo ya Kimataifa hayafuati sheria zinazotoa muongozo wa uandishi habari nchini' na 'kukiuka maadili ya kikazi'.sheria za nchi hiyo kuhusu uanahabari.

Inaishutumu BBC kwa kushindwa kumwajibisha mwanaharakati wa Burundi katika mahojiano aliyofanyiwa katika idhaa ya kifaransa ya shirika hilo.

Radio kadhaa za kibinafasi zimeharibiwa na kufungwa nchini humo wakati wa mzozo wa kisiasa ulizuka mnamo 2015, wakati rais Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais alioshinda baadaye.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini