Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameunda mahakama maalumu kuchunguza mienendo ya jaji wa mahakama ya juu zaidi nchini Kenya Jaji Jackton Ojwang.
Katika taarifa yake maalumu iliyotolewa jana katika Gazette maalumu, Uhuru alisema kuwa kuondolewa mamlakani kwa jaji huyo kutategemea matokeo ya uchunguzi wa mahakama.
Jopo la mahakama hiyo linaongozwa na mwenyekiti wake Justice Alnashir Visram na wajumbe ni majaji (Rtd.) Festus Azangalala, Ambrose Weda, Andrew Bahati Mwamuye, Lucy Kambuni, Sylvia Wanjiku Muchiri na Amina Abdalla.
Rais huyo wa kenya amesema hatua ya kuundwa kwa mahakama maalumu dhidi ya Ojwang, imetokana na ombi lililotolewa na Tume ya huduma za mahakama ya kenya lililowasilishwa kwake na Nelson Oduor Onyango na wajumbe wengine wanane kuhusiana na mienendo ya jaji huyo.
Tume ya huduma za mahakama ilisema aliendesha kesi kaunti ya Migori , wakati ni mshirika wa karibu wa Govana wa kaunti hiyo Okoth Obado
"Katika utekelezaji wa kazi zake, Mahakama itaandaa na kuwasilisha ripoti na mapendekezo kwangu na baada ya hapo nitachukua maamuzi kulingana na mamlaka ninayopewa na sheria ili kutekeleza majukumu yangu ," alisema rais Uhuru.
Aidha rais huyo wa Kenya amemteua Paul Nyamodi na Stella Munyi wote wanasheria, kama washauri ili kusaidia mahakama hiyo maalum kwa ajili ya uchunguzi wa Ojwang.
Alisema Peter Kariuki na Josiah Musili will watahudumu pamoja kama makatibu wa mahakama hiyo maalum.
Katika ripoti ya iliyowasilishwa kwa rais dhidi yake Ojwang anashutumiwa kuwa na mienendo isiyofaa, migogoro isiyoendana na miiko ya kazi yake, na ukiukaji wa kanuni za kazi yake.
Walisema kuwa alikuwa mmoja wa majaji wa mahakama ya juu zaidi walioendesha kesi kaunti ya Migori , wakati ni mshirika wa karibu wa Govana wa kaunti hiyo Okoth Obado.
Wajumbe tisa wa Tume ya huduma za Mahakama nchini Kenya (JSC) walisema Obado aliweka rami kwenye barabara inayoelekea kwenye makazi binafsi ya kijijini ya jaji Obado.
Haki miliki ya pichaREUTERS
Image caption
Katika ripoti ya iliyowasilishwa kwa rais Uhuru kenyatta dhidi yake Jaji Jackton Ojwang( wa pili kulia) anashutumiwa kuwa na mienendo isiyofaa
Kwa maoni yao, Ojwang angepaswa kuifahamisha mahakama na wadau wote juu ya ushirika wake wa karibu na gavana huyo lakini hakufanya hivyo mpaka walipopinga.
"Alipokuwa akiwasilisha ripoti ya kamati ya JSC, tume ilichunguza kwa makini kwa marefu na mapana na kubaini kuwa kuna sababu za kutosha za kumuomba rais kuunda mahakama ya kumuondoa madarakani Justice Jacktone Ojwang, na kuidhinisha ombi kulingana na sheria," alisema Jaji mkuu wa mahakama ya juu nchini humo David Maraga.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments