Meya Awafungisha Ndoa Wapenzi Kabla ya Upasuaji wa Kujifungua | ZamotoHabari.

Meya Awafungisha Ndoa Wapenzi Kabla ya Upasuaji wa Kujifungua
Meya wa Marekani na mgombea wa kiti cha urais ajaye aliwafungisha ndoa wapenzi waliokuja dakika za mwisho tu kabla ya kuelekea hospitali kupata mtoto kwa njia ya upasuaji

Pete Buttigieg, ambaye ni meya wa jimbo la South Bend, Indiana, alisema kuwa wawili hao Mary and Gabe, walimkuta ndio amewasili ofisini majira ya saa mbili unusu na wakamuomba awafungishe ndoa kabla mtoto wao hajazaliwa.

Wafanyakazi wa ofisi ya Meya walikuwa ndio mashahidi na walitumia vipande vya vitambaa( riboni) kama pete kwa kuwa pete zao zilikuwa bado hazijatengenezwa

Baada ya kufunga ndoa yao Mary aliweza kufika hospitalini saa tatu asubuhi kama alivyoagizwa na daktari na kujifungua salama mtoto mchanga wa kike.

Mtoto Jade Katherine Jones amekuwa ''mkazi mpya kabisa'' wa South Bend ",Aliandiika Meya Buttigieg kwenye ukurasa wake wa Facebook.

"Ni nyakati kama hizi ambazo nitazikosa muda wangu wa umeya utakapokwisha ," aliandika alipotuma picha ya mtoto mchanga wa kike.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini