Rais Magufuli Atoa Onyo Kali kwa Wakurudenzi | ZamotoHabari.

Rais Magufuli atoa onyo Kali kwa WakurudenziRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaonya Wakurugenzi ambao watanaoesha nia kudai ushuru kufuatia uamuzi wa Serikali, kununua zao la korosho kwa bei elekezi ya shilini 3300, baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya wakulima na wafanyabiashara wa korosho.

Rais wa Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Mtwara wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara kutoka Mtwara kuelekea Newala na Masasi, ambapo amesema serikali haiwezi kuamua kuwasaidia wananchi halafu Halmashauri ijitokeze kutaka ushuru.

Rais Magufuli amesema, "Halmashauri mmeshindwa kusimamia korosho, baada ya kupewa bei nzuri wanapewa 1500, tukasema hapana tukakopa ili tuwalipe, nione Mkurugenzi ananiomba hizo hela, aone kama ataendelea kuwa Mkurugenzi, utaombea kijijini ukiwa unalima".

Aidha Rais Magufuliamongeza kuwa, "haiwezi Serikali imepanga bei ya korosho 3300, halafu ianze kulipia kodi kwenye Halmashauri ambayo ilishindwa kununua korosho, mkitaka ushuru msimamie vizuri bei ya korosho, siwezi nikakusanya hela mikoa mingine nije niwalipe nyinyi."

Rais Magufuli ameanza ziara ya kikazi Mkoani Mtwara ambapo ameanza April 2, 2019. Amefanya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi kwenye viwanda cha kubangua korosho cha Yalin pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini