Harmonize Afanya Kweli Aamua Kumvisha Pete ya Uchumba Sarah | ZamotoHabari.

Harmonize Afanya Kweli Aamua Kumvisha Pete ya Uchumba SarahMsanii wa Bongo Fleva, Harmonize ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo uitwao 'Kainama' amevisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi, Sarah.

Muimbaji huyo kutokea WCB, ameweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akimvisha Sarah pete hiyo, huko wote wawili wakiwa na nyuso zenye furaha.

Utakumbuka kuwa tukio hilo linakuja siku kadhaa mara baada ya Sarah kuonekana kwenye video ya wimbo wa Harmonize unaokwenda kwa jina la Niteke ambao unapoatika katika EP yake aliyoitoa mwaka huu yenye nyimbo nne pekee.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini