Rais wa Tanzania John Magufuli ameagiza zipelekwe Sh50 bilioni kwa ajili ya kulipia wakulima wenye kilo zaidi ya 1,500 wapatao 18,103 huku akiwasamehe walionunua korosho kwa mfumo wa kangomba.
Magufuli amesema hayo leo Jumanne Aprili 2, 2019 mkoani Mtwara ambako yupo kwenye ziara ya kikazi.
Amesema watakaokiri kuwa walikuwa kangomba na wamefanya hivyo kimakosa tuwaangalie kuwalipa kwa sababu ni wengi akiwamo mwenyekiti wangu wa CCM wa mkoa.
“Kufanya kosa si kosa, ila kurudia kosa ndiyo kosa, lakini nataka wakiri nilinunua korosho sina shamba nilinunua kwa fulani wa namna hiyo walipeni nafikiri watakuwa ni hawa 780 ila wasirudie kwenye msimu unaokuja,”amesema Magufuli na kusisitiza kuwa amewasamehe lakini waandike kuwa walinunua na wana kilo ngapi.
Amesema kwenye uhakiki wa wananchi waliokuwa na kilo zaidi ya 1,500, walikuwa 18, 103 hawajalipwa, waliolipwa ni wachache na uchambuzi wake umekamilika isingekuwa rahisi kutoa fedha bila uchambuzi.
Amesema kati yao yamepatikana majina 780 hawana mashamba wala hawana mkorosho lakini walikuwa wanadai nao wana kilo zaidi ya 1,500.
Amefafanua hao wenye kilo 1,500 ziletwe Sh50 bilioni kuanzia kesho, keshokutwa hawa nao waanze kulipwa, zikiisha zinaletwa nyingine.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments