Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika amejiuzulu wadhifa wake baada ya miaka 20 kufuatia wiki kadhaa za maandamano nchini mwake.
Bouteflika amekuwa madarakani kama rais kwa muda wa miaka 20 , tayari alikuwa amefutilia mbali mpango wa kugombea muhula mwingine kutawala kutokana na kukuwa kwa upinzani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la nchi hiyo, kiongozi huyo tayari aliondoa mipango yake ya kusaka awamu ya tano madarakani, wakati upinzani dhidi ya serikali yake ukiongezeka.
Jeshi la Algeria ambalo lina nguvu, lilimtaka kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kutangaza kuwa hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya uongozi.
Abdelaziz Bouteflika alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi, miaka sita iliyopita na tangu hapo mara chache amekuwa akionekana katika sehemu za umma.
Kujiuzulu kwake kulitangazwa kwa namna gani?
Rais Abdelaziz Bouteflika,aliweza kutoa taarifa hizo rasmi kwa mujibu wa katiba inayoruhusu rais kusitisha muda wake wa kutawala"
Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Uamuzi huo wa Rais Bouteflika ulitangazwa pia na Televisheni ya Taifa ya nchi hiyo.
Kwa nini amejiuzulu?
Msukumo wa wananchi kutaka ajiuzulu ulianza kujijenga tangu mwezi Frebruari, na kusitishwa na tangazo la rais Bouteflika baada ya kutangazwa kuwa hatawania tena nafasi ya uraisi.
Maelfu waliandamana nchini kote tarehe 1 Machi.
Bouteflika amehaidi kuhudumia kama watateuliwa katika awamu ya tano, pamoja na mabadiliko kwa waziri mkuu ambaye alishinwa kuondoka.
Kiongozi wa jeshi ataka rais wa Algeria kuondolewa madarakani
'' Rais wa Jamhuri Bwana Abdelaziz Bouteflika, ametangaza rasmi uamuzi wake wa kumaliza kazi yake kama Rais wa Jamhuri ya Algeria, katika Baraza la Katiba. Uamuzi huo unaanza mara moja kuanzia leo..''
Kuondoka madarakani kwa kiongozi huyo pia kumekuja baada ya kiongozi wa maandamano kukataa ahadi iliyotolewa na Rais Bouteflika wiki hii kwamba atajiuzulu madarakani ifikapo Aprili 28.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments