Wapinzani wa Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya robo fainali, TP Mazembe wametia timu leo kwenye ardhi ya Bongo.
Kabla ya kutua Dar wakiwa kwa ndege yao binafsi ilitua uwanja wa Songwe, Mbeya kwa ajili ya kuongeza mafuta na kufanyiwa maboresho kidogo na kupigwa upepo kidogo wa hapo kabla ya kuendelea na safari ya kuja Dar es Salaam.
Mazembe watamenyana na Simba Uwanja wa Taifa Jumamosi huku kauli mbiu ya Simba ikiwa ni Yes We Can.
Gari ambalo liliandaliwa kwa ajili ya kuwachukua kikosi hicho kimekataliwa na wachezaji hao huku wakipanda magari mengine.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments