Waziri Mkuu Malaysia Apandishwa Kizimbani kwa Ufisadi | ZamotoHabari.

Waziri Mkuu Malaysia Apandishwa Kizimbani kwa Ufisadi
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Razak amekanusha mashitaka yote dhidi yake wakati alipofikishwa mahakamani kuhusiana na kesi ya ulaghai ya mabilioni ya dola.

 Razak mwenye umri wa miaka 65 alikabiliwa na moja kati ya kesi kadhaa kuhusiana na wizi wa fedha za hazina ya kitaifa, inayofahamika kama 1MDB ambao ni mpango wa taifa wa uwekezaji ulioanzishwa kwa ajli ya kuboresha uchumi wa taifa hilo la Kusini mashariki mwa Asia.

 Waziri huyo mkuu wa zamani na washirika wake wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa mabilioni ya dola kutoka kwenye hazina hiyo na kuzitumia katika ununuzi wa majumba ya kihafari, kazi za sanaa ya uchoraji na boti za kifahari.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini