ATSOKO WAADHIMISHA MIAKA 7 TANGU KUANZISHWA KWAKE NCHINI | ZamotoHabari.

*Yajivunia kutoa ajira kwa wanawake, Balozi Sweden ahaidi kuzidi kishirikiana na Tanzania

BALOZI wa Sweden nchini Anders Sjoberg amesema kuwa  ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Sweden utazidi kudumishwa na hiyo ni katika kushirikiana katika masuala ya kiuchumi na kijamii.

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 7 tangu kuanzishwa kwa kampuni ya Kiswedish Atsoko iliyoanza mwaka 2012 kwa duka moja lililopo Mikocheni hadi kufikia maduka 7 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa sasa ambayo yanapatikana  Mikocheni, Slipway-Masaki, Mbezi Beach - Shoppers, Mlimani City, City Mall, Samora Avenue na Quality Centre Anders amesema kuwa wanasherekea miaka 7 ya Atsoko ikiwa na maendeleo lukuki na bado wanaendelea kuangalia njia zaidi za kutoa fursa kwa watanzania kupitia Atsoko.

Amesema kuwa nchini Tanzania soko ni zuri na kumekuwa na ushindani mkubwa hali inayowapa moyo katika kutoa fursa zaidi ili kujenga nchi ya viwanda na kuhusu kutoa ajira Balozi Anders amesema kuwa wamekuwa wakitoa vipaumbele kwa wanawake katika ajira na hiyo ni katika kuwainua zaidi katika suala zima la kiuchumi.

Amesema kuwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili utazidi kuimarika zaidi huku akihaidi kuendelea kushiriki katika kuendeleza shughuli za kijamii na kiuchumi.

Kwa upande wake Meneja mkuu wa Atsoko Tanzania Rehema Julias amesema kuwa, kusheherekea miaka 7 pia  wamezindua bidhaa mpya ya Makeup inayoitwa Note. Ni bidhaa nzuri kutoka Uturuki ambayo inakidhi viwango vya kimataifa na imetengenezwa kwa ajili ya soko la Afrika.

Amesema kuwa kupitia Atsoko vijana na wanawake wamepata ajira na kujiajiri wenyewe huku akiwahakikishia watanzania ubora kwa bidhaa hizo kimatumizi.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjöberg akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Atsoko Tanzania wakati wa hafla ya kusherekea miaka 7 ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo hapa Tanzania iliyofanyika katika duka lao Mlimani City jijini Dar ee Salaam.
Meneja mkuu wa Atsoko Tanzania, Rehema Julius akizungumza kwenye hafla ya kusherekea  miaka saba ya kuanzishwa kwa kapuni hiyo ya vipodozi hapa nchini iliyofanyika katika Duka lao Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya  wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa Atsoko wakifuatilia yanayoendelea kujili kwenye  hafla ya kusherekea  miaka saba ya kuanzishwa kwa kapuni hiyo ya vipodozi hapa nchini iliyofanyika katika Duka lao Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini