Mwisho mwa kituo cha daladala cha Magomeni Mapipa kama ilivyoonekana.
WAKATI mvua zikiendelea kunyesha katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam, leo barabara ya Morogoro hususani eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam lilifungwa kwa mda kutokana na daraja la jangwani kufurika mafuriko hali iliyopelekea mamlaka zinazohusika kufunga barabara hiyo.
Kufa kufaana ndiyo msemo unaoweza kutumika baada ya waendeshaji wa baiskeli za mataili matatu maarufu kama ‘guta’ kuoenekana wakiafanya biashara eneo hilo la jangwani kusafirisha abilia kwa kiasi cha sh. 500 kufika ng’ambo ya pili ili waweze kufika mjiini maeneo ya kariakoo.
Abiria wengi walionekana wakizipata kwa wingi ili kuweza kuvuka eneo hilo pasipokuangalia madahara yanayoweza kuwakumbumba ikiwemo kuanguka kwenye tope.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments