RAIS Magufuli Ashindwa Kujizuia Amwaga Chozi Akiaga Mwili wa Dkt. Mengi | ZamotoHabari.

RAIS  John Magufuli ameshindwa kujizuia na kujikuta akimwaga machozi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi, leo Jumanne, Mei 7, 2019 katika Ukumbi wa Karimjee ambapo zoezi hilo linafanyika.


Magufuli aliungana na familia ya marehemu, marafiki, wafanyakazi wake, ndugu, jamaa na taifa kwa jumla kumwaga mtu ambaye aligusa watu wengi wakiwemo walemavu na watu wenye mahitaji maalum aliokuwa akiwasaidia enzi za uhai wake.


Mwili wa Mengi unaagwa leo Karimjee na kesho Jumatano, utasafirishwa kwenda kwao Machame ambako utazikwa Alhamisi.


Viongozi wengine waliokuwepo ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Makamu wa Rais Mstaafu,  Gharib Bilal;  Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda;  Spika Mstaafu, Anne Makinda; Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma; mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, viongozi wa dini na viongozi wa serikali waliopo madarakani na wastaafu
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini