Jibu la Tanasha kuhusu kujiunga WCB | ZamotoHabari.

Mpenzi Diamond Platnumz, Tanasha ameeleza kama ana mpango wa kujiunga na lebo ya WCB.

Tanasha amesema hana mpango wakujiunga na lebo hiyo baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Radio’.

Mrembo huyo kutoka Kenya ambaye ameonesha kuingia rasmi kwenye tasnia ya muziki baada ya wimbo wake kupokewa vizuri na mashabiki wa muziki Afrika mashariki.

Tanasha amesema mpenzi wake Diamond na timu nzima ya WCB wamekuwa wakimsapoti lakini haoni nafasi yake ndani ya kundi hilo kutokana na aina tofauti ya muziki anayofanya.

 "Nandani aina ya muziki ambayo nafanya ukilinganisha na wasafi ni tofauti kabisa, labda waanzishe wasafi Caribian au Wasafi Hiphop kitu kama hicho, labda,"aliongeza Tanasha wakati akizungumza na Switch Tv ya Kenya.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini