KAMPUNI YA PUMA ENERGY TANZANIA YAWAKUMBUSHA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI KUEPUKA AJALI | ZamotoHabari.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhana(aliyevaa kofia nyekundu) akitoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva waliofika kujaza mafuta katika Kituo cha Mafuta cha Puma jijini Dar es Salaam.Puma imeungana na Shirika la Umoja wa Mataifa kuadhimisha Wiki ya nenda kwa Usalama. Wengine waliokuwa wakitoa elimu hiyo ni wanafunzi wa Shule ya mzingi ambao ni mabalozi wa usalama barabarani.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma  Energy Tanzania imeungana na Shirika la Umoja wa Mataifa kuadhimisha wiki ya usalama barabarani huku kampuni hiyo ikitoa mwito kwa madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabara kwa lengo la kuokoa maisha ya ya watoto.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Puma ni kwamba moja ya vipaumbele vyao ni suala zima la usalama barabarani na ndio maana imeona umuhimu wa kuungana na shirika hilo kubwa duniani kuadhimisha siku hiyo kwa kutoa elimu kwa madereva wa vyombo vya moto nchini Tanzania.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah amewaambia waandishi wa habari kuwa wameamua kuitumia siku hiyo kutoa elimu kwa madareva ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya kimataifa ya nenda kwa usalama barabarani 'UN-Global Road Safety Week (UNGRSW).'

"Puma tumeungana na shiriki hili kutoa elimu ambapo kwetu hapa Tanzania ambacho tumekifanya elimu ya usalama barabarani imetoa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge ambao ni mabalozi wa elimu ya usalama barabarani hususani kwa mkoa wa Dar es Salaam.

"Pia tumeamua kuwatumia watoto kutoa elimu ya usalama barabarani lengo letu Puma ni  kuhakikisha wanaanza kupata uelewa kuhusu masuala ya usalama barabarani. Tupo nao leo kwa sababu hawa ni mabalozi wetu,"amesema Dhanah.

Dhanah amesema kampuni ya Puma Energy itaendelea kushirikiana na taasisi zitakazoendesha mipango mbalimbali ya usalama barabarani kwa lengo la kuhakikisha kuwa watu na vyombo wanavyotumia barabarani wanakuwa salama.

Awali Meneja Programu ya usalama barabarani kutoka Shirika la Neema Swai amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Sema Usikike, Okoa Maisha' na kufafanua maadhimisho hayo huadhimishwa kila baada ya miaka miwili.

"Kila siku watoto ndio wanaotumia barabara kwenda shule na kurudi nyumbani, wasipokuwa na elimu ya kutosha tutawapoteza wengi.

"Mtambue, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), watoto wenye umri kati ya miaka mitano hadi 29, wanapoteza maisha kwa wingi kutokana na ajali, si Malaria wala ugonjwa mwingine ni ajali," amesema Swai.

Amebainisha Serikali inatumia gharama kubwa kumtunza mtoto kunzia miaka 0-5 halafu anakuja kufa kwa ajali ya barabarani kutokana na uzembe wa madereva au kukosa elimu y usalama barabarani, hilo wamelikata na ndio maana wanasema wameamua kupaza sauti.

Mmoja wa wanafunzi walioshiriki kutoa elimu, Godbless Mlacha anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Bunge, amesema wanawashauri  maderva kuacha kutumia vilevi au kwenda mwendo kasi wakiwa barabarani kwa kuwa maisha yao yanakua hatarini.

"Nahitaji kuishi ili nitimize ndoto zangu, uzembe wa dereva unaweza kuondoa uhai wangu au kunipa kilema cha kidumu. Nimechagua kupaza sauti ili kumaliza hili tatizo," amesema Mlacha.

Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeazimia kushirikiana na taasisi nyingine zitakazoendesha mipango mbalimbali ya usalama barabarani kwa lengo la kuhakikisha watu na vyombo wanavyotumia barabarani wanakua salama.

Wakati huo huo baadhi ya madereva ambao wamepata elimu hiyo ya usalama barabarani, wametoa pongezi kwa Kampuni ya Puma kwa jitihada ambazo inachukua kuhakikisha jamii ya Watanzania inakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu elimu ya usalama barabarani.

Wamesema elimu hiyo ambayo inatolewa kupitia wanafunzi ambao ni mabalozi wa usalama barabarani imewahamasisha kuzingatia sheria kwani faida zake ni nyingi ikiwemo ya usalama wa dereva mwenyewe lakini wakati huo huo kuepuka ajali ambazo zinatokana na kutozingatiwa kwa sheria za usalama barabarani.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhana akifafanua jambo kwa moja ya madereva kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria ya usalama barabarani kwa lengo la kupunguza ajali nchini.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam ambao ni mabalozi wa usalama barabarani wakitoa elimu ya usalama barabarani kwa dereva aliyefika kujaza mafuta katika kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Upanga jijini.Utolewaji wa elimu hiyo unafanywa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge ambao ni mabalozi wa usalama barabarani wakitoa elimu ya usalama barabarani kwa mmoja wa madereva aliyefika kujaza mafuta kituo cha mafuta cha Puma kilichopo Upanga jijii Dar es Salaam
 Meneja Programu wa  Usalama Barabarani kutoka Shirika la Amend Neema Swai akielezea ujumbe wa usalama barabarani uliopo kwenye madaftari ya shule ambao unalenga kuwakumbusha wanafunzi na wananchi kwa ujumla kuheshimu sheria za usalama barabarani.
 Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam ambaye ni balozi wa usalama barabarani akitoa elimu hiyo kwa dereva taksi.
Dereva bodaboda akipata elimu ya usalama barabarani kutoka kwa wanafunzi wa shule ya msingi ambao ni mabalozi wa usalama barabarani ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya nenda kwa usalama ya Shirika la Umoja wa Mataifa ambapo Kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania imeungana na shirika hilo kuadhimisha wiki hiyo jijini Dar es Salaam.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini